Sheikh Hemed Jalala: "Mtume (s.a.w.w) ni nuru ya uongofu kwa ulimwengu mzima. Kila Mwislamu anapaswa kujivunia kuadhimisha ujio wake kwa kutenda mema, kujenga amani, na kuendeleza umoja wa Waislamu wote bila kujali tofauti zao".

12 Oktoba 2025 - 14:32

Amani, Umoja, Upendo na Maadili ya Kiislamu: Ujumbe wa Maulana Sheikh Hemed Jalala Katika Uzinduzi wa Maulid ya Mtume (saww) Mkoani Arusha +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Arusha, 11 Oktoba 2025 – Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna‘ashariyyah Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge, ameongoza hafla fupi ya utangulizi wa maadhimisho ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) iliyofanyika jijini Arusha.

Hafla hiyo imeandaliwa na Jumuiya ya Vijana na Wanafunzi wa Dhehebu la Shia Ithna‘ashariyyah Tanzania (TIMSYA), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kitaifa kuelekea kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa Kiongozi wa Uislamu na Waislamu, Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w).

Amani, Umoja, Upendo na Maadili ya Kiislamu: Ujumbe wa Maulana Sheikh Hemed Jalala Katika Uzinduzi wa Maulid ya Mtume (saww) Mkoani Arusha +Picha

Hotuba ya Sheikh Mkuu wa T.I.C

Katika hotuba yake, Sheikh Hemedi Jalala alisisitiza umuhimu wa kuenzi na kuadhimisha tukio la kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu kama fursa ya kurejelea maadili, upendo, na umoja miongoni mwa Waislamu.
Amesema kuwa Maulid si tu hafla ya kihistoria, bali ni jukwaa la kufufua mafundisho sahihi ya Kiislamu na kuimarisha misingi ya udugu wa Kiimani katika jamii.

“Mtume (s.a.w.w) ni nuru ya uongofu kwa ulimwengu mzima. Kila Mwislamu anapaswa kujivunia kuadhimisha ujio wake kwa kutenda mema, kujenga amani, na kuendeleza umoja wa Waislamu wote bila kujali tofauti zao,” alisema Sheikh Jalala.

Amani, Umoja, Upendo na Maadili ya Kiislamu: Ujumbe wa Maulana Sheikh Hemed Jalala Katika Uzinduzi wa Maulid ya Mtume (saww) Mkoani Arusha +Picha

Ushiriki wa Viongozi na Wageni

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kidini, wawakilishi wa taasisi za Kiislamu, wanazuoni, na wanafunzi kutoka vyuo na shule za mkoa wa Arusha.
Washiriki walipata nafasi ya kusikiliza mawaidha mafupi, kaswida, na dua maalum za kuombea amani na mafanikio ya Waislamu nchini Tanzania na ulimwenguni.

Kauli ya TIMSYA

Kwa upande wake, wawakilishi wa Jumuiya ya TIMSYA wamesema kuwa lengo kuu la hafla hiyo ni kuandaa mazingira ya kiroho na kijamii kuelekea maadhimisho makubwa ya Maulid yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mwishoni mwa mwezi huu.

“Tunataka vijana wawe mstari wa mbele katika kusambaza elimu sahihi ya Mtume na Ahlul-Bayt (a.s),” alisema mmoja wa viongozi wa vijana wa TIMSYA.

Amani, Umoja, Upendo na Maadili ya Kiislamu: Ujumbe wa Maulana Sheikh Hemed Jalala Katika Uzinduzi wa Maulid ya Mtume (saww) Mkoani Arusha +Picha

Hafla imehitimishwa kwa dua maalum ya umoja na mafanikio ya Taifa, huku Sheikh Mkuu akihimiza mashirika na jumuiya zote za Kiislamu kushirikiana katika kudumisha amani, upendo, na ustawi wa jamii.

Your Comment

You are replying to: .
captcha